KIFO CHA RAY C CHA NUKIA
Staa anayetamba na ngoma mpya ya ‘Nshumu nshumu’, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Staa
anayetamba na ngoma mpya ya ‘Nshumu nshumu’, Rehema Chalamila ‘Ray C’
hivi k aribuni alijikuta katika wakati ngumu baada ya kuvamiwa na paka
na kumng'ata kwenye mguu.
Sosi
wa habari hii alisema kuwa Paka yule alikuwa eneo la Methadone
Mwananyamala Hospitali ambapo mwanamuziki huyo anakunywa dawa.
“Alipopita Ray C alirukiwa na paka na kumgangania mguu alijaribu kumzuia lakini hakufanikiwa kitendo kilichozua utata kwani bila watu kumsaidia paka yule asingetoka mguuni kwake”, alisema Sosi.
Aidha
Sosi huyo alisema kuwa baada ya paka huyo kumvamia mambo yake yamekuwa
magumu ni mtu ambaye anaomba hata mia tano na kwa sasa amefunga
mghahawa wake.
“ Yaani Ray C kwa sasa anatia aibu kwani maisha yamemharibikia mpaka watu wanadai kuwa huenda yule paka hakuwa wa heri, amekuwa mlevi anavuta sigara ovyo mpaka mwenye nyumba wake hamtaki tena nadhani mkataba wake umesitishwa”, alisema Sosi.
Baada
ya habari hizi kutua kwenye meza ya Ijumaa mwandishi alimwendea hewani
Ray C ambaye alikiri kuvamiwa na paka na kudai kuwa yeye haamini kama
unaweza kuwa ni uchawi anahisi alimkanyaga mkia bila kujua.
