JANGILI WA KIMATAIFA AKAMATWA TANZANIA
Feisal Mohamed Ally Polisi wa kimataifa , interpol tawi la Tanzania
wamemkamata mfanya biashara maarufu raia wa Kenya kwa tuhuma za
kujihusisha na ujangili na uhalifu uliovuka mipaka ,hususan mauaji ya
tembo . mtuhumiwa huyo Mohamed Ally Feisal Amekamatwa mjini
Dar-Es-Salaam baada ya kusakwa kwa kipindi kirefu kwa makosa hayo ya
kimataifa kutoka Dar Regina Mziwanda anaarifu zaidi. Akitbibitisha
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Bwana Diwani Athumani kutoka kamisheni ya
Kurugenzi ya makos aya jinai amesema mtuhumiwa huyo anakabiliwa na
tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kimataifa ikiwemo
uwindaji wa uliovuka mipaka kimataifa katika nchi mbali mbali) Bwana
Athumani Diwani alieleza kuwa kwa sasa mtuhumiwa huyo anashikiliwa huku
upelelezi ukiendelea kujua makosa mengine aliyoyafanya kuhusiana na
biashara za bidhaa zitokanazo na Tembo ndani ya Tanzania na katika nchi
nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo nchi yake ya asili Kenya. Mohamed
Feisal Ally amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za uwindaji
haramu husani mauaji ya Tembo tatizo ambalo ni kubwa hususani katika
ukanda huu wa Afrika Mashariki hasa Kenya na Tanzania ambapo idadi kubwa
ya Tembo wamekuwa wakiuawa kila mwaka na kutishia kutoweka kwa viumbe
hao.