GORAN KUVUNJA UCHAWI WA SIMBA
KOCHA mpya wa Simba raia wa Serbua Goran Kopunovic amemwaga wino wa mwaka mmoja kuinoa timu hiyo ya Msimbazi.
Mmoja
wa viongozi wa Simba aliiambia blog ya jamii kuwa kocha huyo
aliyewasili leo asubuhi na kufikia kwenye hotel ya Double Tree Masaki
ataondoka kesho kwenda Zanzibar kujiunga na timu hiyo ya wekundu wa
Msimbazi inayoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Naye
Kopunovic akizungumza muda mfupi baada ya kukanyaga hardhi ya Tanzania
alisema "Nimekuja kufanya kazi, naamini nitapata ushirikiano kutoka kwa
viongozi wa Simba, wachezaji na mashabiki, Simba ni timu kubwa,
naamini nitawapa mafanikio."alisema
Kocha
huyo, amechukua mikoba ya Patrick Phiri aliyefungashiwa virago baada
ya uongozi wa Simba chini ya mwenyekiti wake Evans Aveva kufanya
tathmini ya mwenendo wa timu ambapo ametoka sare mechi sita, ameshinda
mechi moja na kupoteza moja hivyo kuona hastaili kuendelea kuinoa timu
hiyo ya mtaa wa Msimbazi huku akidaiwa kukaidi agizo la viongozi la
kutowachezesha Waganda katika mechi dhidi ya Kagera walionyukwa bao 1-0
