DUDE ATOA SIRI YA WASANII WENYE NGOMA BONGO MOVIES
Staa wa Filamu za Kibongo, Kulwa
Kikumba ‘Dude’ ameibuka na kusema kuwa kuelekea mwisho wa mwaka mastaa
wengi wana ngoma na mbaya zaidi wanaambukizana wao kwa wao.
Akizungumza na Ijumaa, Dude alisema kuwa mastaa wazima ni wa kuhesabika na kutaja sababu kubwa kuwa ni kubadilishana na kuibiana wapenzi bila kuwa na woga .
Akizungumza na Ijumaa, Dude alisema kuwa mastaa wazima ni wa kuhesabika na kutaja sababu kubwa kuwa ni kubadilishana na kuibiana wapenzi bila kuwa na woga .
“Utakuta
Mbongo Fleva ana mtu kwenye Bongo Muvi na Mbongo Muvi ana mtu kwenye
dansi au kwa mamis au hata wacheza mpira, ukitaka kuujua ukweli tangaza
dau kuwapima mastaa uone watakaojitokeza,” alisema Dude.
Aidha,
Dude alisema anavyoona yeye ingeanzishwa kampeni ya mastaa wa Bongo
kupima Ukimwi kwani anawahofia watoto wa kizazi kipya zaidi ambao
wanajikuta wanaingia pabaya na kuzima ndoto zao.