BABY MADAHA ASEMA BILA MAPENZI HAWEZI KUFANYA LOLOTE
Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha.
Stori: Gladness Mallya
MWANADADA asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha ameibuka na kutoa kali ya mwaka kwamba anapenda mapenzi kuliko kitu kingine chochote duniani.
MWANADADA asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha ameibuka na kutoa kali ya mwaka kwamba anapenda mapenzi kuliko kitu kingine chochote duniani.
Akichezesha
taya na paparazi wetu, Baby Madaha alisema ‘hobi’ yake ni mapenzi
japokuwa anapenda muziki lakini haifikii jinsi anavyoyapenda mapenzi
kwani yanampumzisha akili yake na kumfurahisha moyo wake pia.
“Ukweli
napenda mapenzi kuliko kitu chochote ila sipendi kuzinguliwa na
wanaume, ninapenda muziki, filamu lakini haviwezi kufikia mapenzi kwani
ndiyo kila kitu kwangu na yananipa starehe kuliko kitu chochote hapa
duniani,” alisema Baby Madaha.