MSUVA AIONGOZA YANGA IKIIBUKA NA USHINDI WA GOLI 4 MBELE YA JKT RUVU



Mshambuliaji wa yanga Saimon Msuva hii leo ameiongoza timu yake kuibuka na ushindi wa goli 4-0 mbele ya JKT Ruvu yeye akifunga goli 2 katika ushindi huo mnono, unaowaweka kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya vodacom kwa pointi 1 zaidi ya Simba SC na Azam FC.

Katika mchezo huo yanga sc walienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0, zilizofungwa na Saimon Msuva katika dakika ya 12 na Issoufou Bobackari katika dakika ya 43 ya mchezo.

Yanga SC walianza mchezo kwa kasi na kuonyesha dhamira ya kutaka kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo lakini ilibidi wangoje mpaka dakika ya 12 goli la Saimon Msuva kuwapa uongozi huo.

Kuingia kwa goli hilo kuliwaimarisha JKT Ruvu lakini yanga SC walikuwa na kasi zaidi pale wanapo saka goli katika mchezo huo wa leo ambapo walienda mapumziko wakiwa mbel kwa goli 2-0.

Katika kipind cha pili Yanga SC waliendeleza kasi yao ya kusaka goli huku JKT Ruvu wakitolea na kutafuta goli taratibu,

Katika dakika ya 62 Donald Ngoma aliiandikia Yanga SAC goli la 3 kabla ya Saimon Msuva kuhitimisha katika dakika 3 za nyongeza na kupelekea mchezo kumalizika kwa yanga sc kuibuka na ushindi wa goli 4-0,

Kwa matokeo hayo Yanga SC wamefikisha pointi 43, wakibakia katika usukani wa ligi wakifuatiwa kwa karibu na Simba SC na Azam FC wenye pointi 42 kila mmoja
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.