MGAMBO COASTAL WAENDELEA KUPOTEZA, MAJIMAJI AKISHINDA
Kikosi cha Mgambo shooting kilichocheza na Simba SC juma lililopita
Vijana wa kocha Bakari Shime Mgambo Shooting hali imeendelea kuwa mbaya kwao baada ya leo kukubali kichapo cha goli moja bila toka kwa majimaji FC, mchezo uliochezwa mjini Songea.
Kichap hicho cha goli 1-0 toka kwa Majimaji FC ni muendelezo wa matokeo mabovu waliyokuwa wanayapata katika siku za karibuni ambapo katika michezo 4 wameambulia pointi 1 pekee.
Wakati Mgambo shooting wakikbulai kichapo jirani zao Coastal union nao wamekubali kichapo cha goli 2-1 toka kwa Coastal union, ikiwa ni muendelezo wa jinamizi la kuifunga yanga sc.
Coastal union toka waifunge yanga sc wamecheza michezo miwili ambapo wamepoteza yote hiyo.