AZAM FC WATWAA UBIGWA ZAMBIA
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, jioni ya leo imetwaa ubingwa wa michuano maalumu iliyomalizika jijini Ndola Zambia baada ya kutoa suluhu dhidi ya Zanaco FC ndani ya Uwanja wa Levy Mwanawasa.
Sare hiyo imeifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi tano sawa na washindi wa pili Zanaco, lakini imewazidi washindi wa pili hao wa Ligi Kuu Zambia, kwa wastani wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam FC kama ingekuwa makini kwenye mchezo huo huenda ingejiandikia bao la uongozi dakika ya 8 baada ya kufanya shambulizi kali langoni mwa Zanaco, lakini shuti alililopiga Kipre Tchetche nje kidogo ya eneo la 18, lilipanguliwa na kipa na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.