NEWS ALERT: WASHABIKI WA TIMU YA SIMBA WAPATA AJALI MKOANI MOROGORO LEO
Ajali
mbaya imetokea leo maeneo ya Makunganya, Barabara kuu ya kutoka
Morogoro kwenye Dodoma baada ya gari iliyokuwa imewabeba washabiki wa
Timu ya Simba Sports Club kupoteza muelekea na kuingia porini, watu nane
wamepoteza maisa na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya.
Hili ni pigo kubwa sana kwa Timu ya Simba, tutaendelea kupeana taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
Globu
ya Jamii inatoa pole wa Klabu ya Wekundu wa Msimbazi kuwa kuondokewa na
washabiki wake hao, na Mungu aziweke Roho za Marehemu hao mahala pema
Peponi, Amin.
Zoezi la uokoaji wa watu waliokuwa ndani gari hilo ikiendelea.
Muonekano wa gari hilo baada ya ajali.
