SIMBA AZAM NOUMA ZAENDELEZA UBABE TAZAMA ILIVYOKUA
Simba SC na Azam FC wameendelea kunganganiana baada ya leo kila mmoja kuibuka na ushindi wa goli 1-0 katika michezo yao ya ligi kuu, na kuifanya Simba SC kuendeleea kukalia kiti cha pili wakitofautiana na Azam FC kwa wastani wa magoli mawili.
Katika uwanja wa Kambarage Simba SC walikuwa wageni wa Kagera sugar ambao walikuwa hawajapoteza mchezo toka wahamie katika uwanja huo wa CCM Kambarage wakitokea katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Tabora.
Katika mchezo huo goli la Simba SC lilifungwa na Ibrahim Ajibu katika kipindi cha kwanza huu, na kuipeleka Simba Sc mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Katika kipindi cha pili Simba SC waliapata penati ambayo Ibrahim Ajibu alikosa penati hiyo, ikiwa ni kabla ya mchezaji wa Kagera sugar kuzawadiwa kadi nyekundu katika dakika ya 80 ya mchezo na kupeleka mchezo kumalzika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Kiujumla Simba SC walipoteza nafasi kadha za kufunga magoli huku wakitawala mchezo katika vipindi vyote viwlili vya mchezo.
Katika uwanja wa Azam Complex, Azam FC wao walikuwa wenyeji wa Mwadui FC na mchezo huo ulimalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililo fungwa na Kipre Herman Tcheche.
Katika mchezo huo Mwadui FC hawakuwa na bahati, walitengeneza nafasi nyingi za wazi lakini walishindwa kuzitumia na kupelekea ushindi ubakie hapo Chamanzi.